Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mkuu Majaliwa awageukia waliotafuna fedha za shirika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitahusika na ulipaji wa deni la fedha za Ushirika na badala yake kila aliyekula fedha hizo atazilipa mwenyewe.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa wilaya.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika na ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, amesema Serikali haiwezi kukubali Ushirika ukafa nchini kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa waaminifu.

Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuongoza Vyama vya Ushirika na kuamua kujinufaisha kwa kula fedha za vyama watazilipa.

Waziri Mkuu amewaagiza Viongozi wa Mkoa wa Lindi kufanya ukaguzi katika Vyama vyote vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) ili kubaini ni wakulima wangapi wanadai.

Amesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini idadi ya wakulima wanaodai na kiasi cha fedha wawachukulie hatua wahusika wote kwa mujibu wa sheria.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top