Jeshi la Polisi Kanda Malaam ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi nane wanaodaiwa kuendesha mtandao wa wizi wa magari sehemu mbalimbali za jiji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lucas Mkondya, amesema watu hao wamekamatwa huko Kongowe mkoa wa Pwani wakiwa na gari moja aina ya Noah lenye namba T 455 DEP.
"Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao na kuwahoji wamekiri kuendesha mtandao wa wizi wa magari katika jiji la Dar es Salaam na sehemu nyingine za nchi na mpaka sasa wamekiri kuiba magari mengi". Amesema Mkondya.
Ameongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao ili kupata taarifa za watu wanaowauzia magari hayo baada ya kuyaiba pamoja na mtandao mzima wa wizi huo ili kudhibiti wizi wa magari Dar es salaam.
"Tunaotaka kuwabaini hasa ni wanunuzi wa hayo magari lengo ni kusambaratisha mtandao huo ila lengo ni hao wanunuzi ambao ndio hasa tunawatafuta," amesema Mkondya.
Alfajiri
1 hour ago
Post a Comment