Loading...
Cheyo 'amvaa' Lowassa
Cheyo amtaka Lowassa kuacha uchochezi
Mwenyekiti wa UDP John Cheyo amemjia juu Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya RICHMOND Edward Lowassa na kumtaka aache kauli za uchochezi.
Ingawa Cheyo hakumtaja jina, lakini kauli zake zilionekana wazi kumlenga Lowassa ambaye siku za karibuni ametoa kauli zenye kuchochea mfarakano wa kidini.
Mwenyekiti huyo alisema mtu ambaye amekuwa Waziri Mkuu na akatoka kwasababu mbalimbali kama kustaafu au kujiuzulu, anapaswa kutoa mchango kwa nchi.
Cheyo alisema, Waziri Mkuu mstaafu anapaswa kutoa matamshi ya kupatanisha watu badala ya kuwagawa na kuvuruga amani.
"Ukitaka nchi iharibike, ipate matatizo, ingiza mambo ya dini, ukianza kuzungumzia mambo ya uhamsho, ni yanayoleta hisia za kukwazana kidini" alisema Cheyo.
Aidha, Cheyo alitoa wito kwa mawaziri wakuu akiwemo Lowassa ambaye anaishi kwa kodi ya wananchi kwa asilimia 80 ikiwemo kupata matibabu, anapaswa kuangalia vitu vya kuzungumza ili kulinda amani ya nchi.
Post a Comment