Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HALI TETE CHADEMA ..... VIGOGO WAKIMBILIA KUJIUNGA CCM



Mwenyekiti wa mtaa wa Isegenge kata ya Mandu jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza ndugu Gidion Msusu leo amekihama Chama chake cha CHADEMA na kuuungana na waungwana wa CCM kuhakikisha kuwa wanaipa Serikali muda wa kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa.

Huu ni mwendelezo wa hama hama unaosababishwa na kutokuwa na vyama imara vya upinzani vyenye siasa za chuki, vitisho na vyenye kila dalili ya ukanda, udini na ukabila.

Sambamba na hayo, utendaji MZURI wa Rais JPM umeendelea kuwafanya watu wenye akili timamu kuachana na siasa uchwara na kuamua KUMUUNGA mkono Rais wetu mpendwa John Joseph Pombe Magufuli.

Ilianza kama mchezo baada ya ALIYEKUWA KATIBU wa CHADEMA MKOA wa Mwanza Mwana wa Nzwalie John Thobius Nzwalile kukiacha Chama hicho na baadae kufuatiwa na viongozi wengi waandamizi wa Chama hicho kama Damas Kimenyi, ALIYEKUWA KATIBU wa wilaya Ilemela, Joseph Warioba ALIYEKUWA MKURUGENZI wa usalama wa CHADEMA KANDA ya ziwa, Hamis Tabasam, George KAYEGO, Mwl Nicky Maige, Kamanda John Haule John na wafuasi zaidi ya 800.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top