Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kizaazaa Dar mwanamke ‘atua’ uchi Airport

MWANAMKE mkazi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye jina lake halikufahamika, amesababisha kizaazaa jijini, baada ya kushuka na ungo akiwa uchi wa mnyama.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na kushangaza watu kadhaa waliokuwa na taharuki, lilitokea juzi karibu na eneo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA).

Katika tukio hilo ambalo lilitokea majira ya mchana, mwanamke huyo alianguka katikati ya barabara katika eneo la  Ukonga Banana wilayani Ilala, akiwa kwenye ungo wake ambao alikuwa ameukalia bila kuvaa nguo.

Mwanamke huyo alikutwa amevaa sidiria yenye rangi nyeupe na kichwa alikuwa amefunga kilemba chenye rangi nyeupe.

Picha za mwanamke huyo zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na video akionekana amekaa katikati ya barabara.

Ungo aliokuwa ameukalia ulikuwa na unga huku akionekana akiongea na simu. Pia na kwenye masikio yake alionekana amevaa earphones.

Baada ya kugundua yupo katikati ya barabara, alinyanyuka na kwenda kuokota mizigo yake mingine ambayo ilianguka kandokando ya barabara hiyo, ukiwamo mkoba na viatu.

Makundi ya watu kadhaa walianza kumfuata huku mwanamke huyo akikimbilia kwenye kiwanja kilichopo TAA akiwa anajaribu kujificha viongo vyake visionekane kisha alichukua gauni lililokuwa kwenye begi na kuanza kulivaa.

Baada ya kuvaa, watu walianza kumzonga na kumzomea wakimuita mchawi na wengine wakaanza kumtembezea kichapo huku wakimuita mchawi.

“Mwanga, mchawi, muulize anatoka wapi. Kama ni mgonjwa mbona una zana… mchawi, mwanga,” walisikika wakimzonga.

Nipashe ilizungumza na mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini na kueleza kuwa mwanamke huyo anaishi karibu na Banana.

“Nimeelezwa anapoishi sio mbali, kumbe anajulikana na baadhi ya wanaomjua wamemshangaa kukutwa na tukio hilo lenye imani za kichawi, cha ajabu zaidi ameadhirika mchana,” alisema.

Taarifa ambazo hazikuthibitishwa zilidai kuwa mwanamke huyo alichukuliwa na Polisi kwa lengo la kumuokoa dhidi ya kichapo zaidi kutoka kwa wananchi waliokuwa na hasira.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, alipoulizwa jana kuhusiana na tukio hilo, alisema halijaripotiwa katika kituo chochote cha polisi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top