Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Halima Hassan amefariki dunia asubuhi hii, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali.
Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinums, amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram, na haya ndiyo ameyaandika;
Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.
Post a Comment