USIKU wa kuamkia leo ilikuwa ni shangwe kwenye Ukumbi wa Mlimani City wakati wa sherehe ya Rapper nguli wa Bongo ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’ aliyefunga ndoa jana hiyohiyo Julai 8, 2017 na mpenzi wake Grace katika Kanisa la St. Joseph lililopo Posta ya Zamani Dar.
Licha ya Sherehe hiyo kuhudhuriwa na watu mashuhuri wakiwemo wabunge, Basi Ridhiwani Kikwete ameandika maneno haya kupitia ukurasa wake wa Instagram...
"hata Ubuyu ulianza kama Jay Mwisho ukakatika." Prof. Jeezy nawe umeaga kambi ya Mabachela na umejiunga na kambi ya Wastaarabu. Hongera sana Brother. Nisamehe kwa kushindwa kuhudhuria kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Nakujali sana bro.@professorjaytz"
Post a Comment