Na Mwandishi Wetu, Tanga
Umoja wa Viijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umewashauri wanafunzi wanaohitimu Vyuo na Vyuo Vikuu kuzitumia fani na elimu zao ili kufanya tafiti za kitaaluma kulingana na changamoto zilizopo nchini na matokeo ya tafiki hizo zitowe majawabu chanya yatakayonyesha njia mbadala za kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.
Umoja huo pia umewataka wasomi hao kuendelea kuukiunga mkono chama cha mapinduzi na serikali zake kwa minajili ya kuwaendeleza kitaaluma, kifikra na kifalsafa huku mioyo yao ikijengeka kwa rutuba za uzalendo na kujitegemea.
Ushauri huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Vyuo na Vyuo vikuu waliohitimu Korogwe mkoani hapa.
Shaka alisema elimu walizonazo wanafunzi hao wa vyuo na vyuo vikuu na waliofuzu fani mbalimbali zinahitaji kutumiwa kwa maslahi ya kuisaidia nchi katika maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kujiajiri huku akiwaasa wasivunjike moyo badala yake elimu zao ziwajengee ujasiri na kujiamini.
Alisema ni wajibu wa kila kijana msomi kutafakari kwa kina na kutumia elimu walizonazo ili kujitegemea, kujiamini na kubuni mambo ambayo yatawasaidia wao na nchi kutoka hatua moja hadi kufika nyingine kimaendeleo.
"Mmepata bahati ya kupata elimu ngazi za ya Vyuo na Vyuo Vikuu, onyesheni njia kwa kutumia elimu hizo ili kufanyeni tafiti za kitaaluma ambazo zitakazoonyesha njia, majawabu na kujibu maswali ya changamoto zilizopo na kuonyeaha njia mbadala "Alisema.
Aidha Shaka akiwahimiza wahitimu hao kuiga uzalendo, ujasiri na moyo wa kujituma kama anavyotekeleza Rais John Magufuli kwa kuitumikia nchi usiku na mchana kwa manufaa ya pamoja huku akionyesha mfano wa uongozi bora.
"Tunakishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kutuletea Rais mzalendo na mchapakazi, Rais Dk Magufuli hana budi kuungwa mkono kwa jinsi anavyojitoa na kutimiza wajibu wake kwa nchi na Taifa lake, wasomi wa vyuo na vyuo vikuu ni wakati wenu nanyi kuiga mema haya na kujifunza "Alisisitiza.
Pia kaimu huyo katibu mkuu aliwataka wahitimu hao kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu za kuwania uongozi ndani ya jumuiya kwani wakati huu wa uchaguzi jumuiya na Chama kinahitaji kupata viongozi ambao ni warithi wa uongozi ujao kisiasa na kiserikali.
Shaka aliwataka kuitumia nafasi hiyo ili wasomi hao wakichaguliwa waweze kuonyesha uwezo, maarifa walionayo, elimu zao kwa kuiendeleza nchi katika maendeleo ya kisekta huku akiwaasa na kuwataka kujua kuwa hakuna chama mbadala cha kuiondosha ccm madarakani.
"Hamtajuta kujiunga na CCM kwani ndicho chama pekee bora chenye sera makini, historia safi, viongozi bora , tambueni haitatokea siku moja CCM kushindwa uchaguzi kwasababu ni chama kinachojali na kupigania maslahi ya umma, angalieni kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano tayari inatuonyesha njia ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2020 chini ya Dk Magufuli "Alieleza huku akishangiliwa.
Jumla ya wanafunzi 1,260 wamehitimu katika vyuo na vyuo vikuu mbali mbali mkoani Tanga walishiriki katika hafla hiyo.
Mapema Kaimu Katibu Mkuu Shaka Akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Injinia Gabriel alikagua ujenzi wa shule za msingi za kisasa unajengwa kwa nguvu za wananchi na serikali ya Wilaya ya Korogwe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM 2025-2020.
Post a Comment