Serikali imesema kuwa imepunguza bei ya vifaa mbalimbali vinavyotumika katika sekta ya afya zikiwemo bei za dawa, vitendea kazi na vifaa tiba vya maabara vinavyonunuliwa na kusambazwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa asilimia 15
Hayo yamesmwa jana na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Bahari ya Dawa (MSD) ambapo alisema kuwa hayo ni matokeo ya utaratibu wa kuanza ununuzi wa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji kama Rais Dkt. John Magufuli alivyoagiza.
Alisema kuwa kwa sasa Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya vianapaswa kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa na Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
“MSD kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania,”alisema Ummy Mwalimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh, India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Hata hivyo, kwa upande wa vifaa tiba alisema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.
Post a Comment