Loading...
MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM
sasa *10* kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi *Million 400* kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya *TONGBA* ya China.
Hatua hiyo inakuja baada ya *RC Makonda* kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza *Misafara* ya Viongozi, *Misiba* na kuwahisha *Wagonjwa* waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.
*Makonda* amesema lengo lake ni kuboresha *Mazingira* ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha *Askari* wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata *Baiskeli 500*, *Pikipiki za kawaida 200* *Computer 100* , *Pikipiki za Trafic 10* na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.
Aidha *Makonda* amemuagiza aliekuwa *Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam* kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa *Dawa za kulevya* na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.
Agizo hilo limekuja baada ya hivi juzi Msamariamwema kutoa taarifa za uwepo wa muhusika wa Dawa za kulevya kwenye moja ya Hotel na Askari walipofika kwenye Hotel hiyo wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda Mtuhumiwa akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel kisha kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia *Camera za CCTV* wakawabaini Askari hao.
Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi cha *Million Tano* iliwasisambaze Picha hizo kitendo ambacho ni kinyume Sheria ambapo Mheshimiwa *Makonda* amesema hawezi kuruhusu vitendo kama hivyo vitendeke kwenye Mkoa wake na kuongeza kuwa anataka kuona Sheria na Haki vinatendeka kwa Wananchi.
*Makonda* pia amebaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanaowabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.
Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya *Jeshi la Polisi* na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.
Post a Comment