Msanii wa filamu za bongo ambaye mara nyingi husemwa vibaya kutokana na pengo lake la pembeni, amefunguka na kusema pengo hilo aliliweka makusudi ili kumridhisha aliyekuwa mpenzi wake.
Akipiga stori na Big Chawa wa Planet Bongo ya East AFrica Radio, Jackline Wolper alisema mpenzi ambaye alikuwa naye wakati huo alikuwa anapenda mwanamke aliye na mwanya lakini yeye hakuwa akipenda mwanya, hivyo akaamua kung'oa jino hilo la pembeni ili amridhishe mpenzi wake.
Wolper aliendelea kusema kwamba jino hilo aling'oa akiwa nchini Afrika Kusini alikoenda na mpenzi wake huyo, na ndiye aliyemlipia gharama za kufanya hivyo na kuweka jino la dhahabu, lakini pamoja na kufanya hayo yote mpenzi wake huyo hakufurahia, kwani yeye alitaka mwanya.
Loading...
Post a Comment