Rais John Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa 33 wa kawaida wa Jumuia ya Tawala za Mitaa (Alat).
Mwenyekiti wa Alat, Gulamhafeez Mukadam amesema, awali mkutano huo ulipangwa kufanyika Septemba 19 hadi 22 lakini kutokana na baadhi ya wanachama kutokusanya fedha kwa wakati, umesogezwa na sasa utafanyika Oktoba 2 hadi 5 mkoani Mbeya.
Amesema kutokana na mamlaka za Serikali za mitaa kuwa wanachama wa Alat na Rais ndiye mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, hivyo atakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.
Amesema pamoja na mambo mengine, mkutano huo ni fursa ya kuwakutanisha viongozi wakuu wa Serikali Kuu na za mitaa kwa ajili ya kutoa maelekezo na miongozo ya kisera kwa watekelezaji ambao ni mamlaka ya serikali za mitaa nchini.
Mukadam amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ardhi kwenye mamlaka ya Serikali za Mitaa ni chachu ya maendeleo, halmashauri zitenge ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogovidogo na vikubwa".
Amsema," Tutatumia mkutano huu kujikita zaidi katika suala zima la uwekezaji katika viwanda kwa kuhakikisha halmashauri zinakuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za kuwa na Tanzania ya viwanda."
Loading...
Post a Comment