Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mkuu Awataka Wawekezaji Kufuata Sheria

Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu. 

Ametoa kauli hiyo jana Jumanne, Agosti 29, 2017 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa kampuni ya PIRIOU, Bw. Michel Perrin.

 Waziri Mkuu alikutana na Bw. Perrin jijini Paris nchini Ufaransa kupitia ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. 

Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli. 

Akizungumza na muwekezaji huyo Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini. 

“Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi.Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo nakukaribisha sana.”

 Kwa upande wake Bw. Perrin alisema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba anauhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jiraji. 

Alisema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi.

 Pia Bw. Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samwel Shelukindo kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini. 

Naye Balozi Shelukindo alisema atahakikisha anaendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top