Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

AJIRA MPYA, MADARAJA YAMEPANDA, MISHAHARA IMEONGEZEKA

Ni utaratibu wa kawaida uliozoelekea kwa Watumishi wa umma kupandishwa madaraja ama mishahara kuongezwa. Hii hufanywa na Serikali kila mwaka mpya wa bajeti unapoanza lakini mshangao mkubwa umejitokeza tangu Serikali ya awamu ya 5 iingie madaraka mwaka 2015, haikusikika kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 mishahara ikipanda wala madaraja yakiongezwa ama ajira mpya zikitangazwa.
Imezua gumzo hili kutokana na kuwa na mazoea tuliyojiwekea. Lakini tangu Serikali ya awamu ya 5 yake Rais Dokta John Pombe Magufuli iingie madarakani mwaka 2015 ilianza na zoezi la kusitisha kutangaza ajira mpya zote, upandaji wa madaraja na nyongeza za mishahara kwa sababu kubwa kuu moja ya kufanya uhakiki kwa Watumishi wa umma.
Tumeshuhudia, tumesikia na kuona uhakiki ukifanywa ili kuwabaini wote wenye vyeti feki na wenye majina vyeki ambapo mwisho wa siku ripoti ikatolewa. Aprili 28, mwaka huu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Angella Kairuki, alimkabidhi Rais Dk. John Magufuli majina 9,932 ya watumishi wanaodaiwa kuwa na vyeti feki.
Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Rais Dkt Magufuli aliagiza watumishi hao kuondoka wenyewe kazini hadi ifikapo Mei 15, mwaka na wasipofanya hivyo watafikishwa mahakamani.
Zoezi la uhakiki liliendelea ambapo mpaka sasa zaidi ya ajira feki laki mbili zilipatikana ambao hao ni wale wenye vyeti feki, majina feki, waliopata kazi kinyume na utaratibu.
Bila ya Serikali kuanzisha msako huu mkali hali ingeendelea ya Watu wasio na sifa kuziba nafasi za Watu wenye sifa zao, wenye elimu ya kutosha ambao wanazagaa mitaani na tatizo la ajira kuzidi kuongezeka nchini. Pia ingekuwa kazi kubwa Serikali kutangaza ajira mpya wakati ambao wanafanya uchunguzi kubaini wenye vyeti.
Mara baada ya kuwepo kwa nafasi wazi tele za ajira na zoezi la uchunguzi kukamilika, Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, imetangaza nyongeza ya mshahara na kutangaza ajira mpya.
“Tayari Serikali imeshatenga Tsh. Bilioni 600 kwa ajili ya kuanza kupandisha madaraja wafanyakazi wote ambao wanastahili,” amesema Waziri Angella Kairuki Septemba 5, 2017 akiwa Bungeni mjini Dodoma.
Waziri Angella Kairuki amesema amesha saini vibali 11,000 kwa ajili ya ajira mpya na vibali 40,000 kwa ajili ya ajira mpya nyingine tena atazisaini tena hivi karibuni na hivyo kufanya ajira mpya zitakazotolewa kuwa zaidi elfu hamsini (50,000). Kipaumbele kikubwa ni kujaza nafasi za Waalimu na watu wa idara ya afya ambao ndio waathirika wakubwa wa vyeti vyeki.
Wahenga walisema; “Mvumilivu hula mbivu”. Sasa Watanzania wanaona matunda ya uhakiki wa ajira ambapo nafasi mpya zaidi ya laki Mbili(200,000) zimepatikana na hivyo kutapunguza tatizo la ajira kwa wasomi , kiwango cha utegemezi kwenye jamii na famii kitapungua, mawazo mapya na nguvu mpya ya kusukuma gurudumu la maendeleo nchini yatapatikana. Yote hayo ni matunda ya subira na uvumilivu wakati Serikali inapokuwa kwenye utendaji.
Ahsante Rais Dkt Magufuli na Serikali yako ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupandisha madaraja Wafanyakazi wote wanaostahili, kuongeza mishahara na kutangaza ajira mpya hali itakayopelekea kupunguza tatizo la ajira nchini kwa vijana.
Image may contain: 1 person, sitting
Na Emmanuel J. Shilatu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top