Mwanamitindo ‘hot’ ambaye kwa sasa amegeuka mswaki kutokana na kuongelewa kila kona, Hamisa Mobetto, amewaacha watu njia panda baada ya kupost picha ya gari aina ya Prado yenye thamani ya zaidi ya milioni 50, mashabiki wanadai baada ya ile Rav 4, hiyo ni zawadi nyingine anatarajia kupewa na mzazi mwenziye ambaye ni Mbongo Fleva aliyezaa pia na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Mobetto aliposti picha ya gari hiyo na kuandika jina la mtoto wake.
“Dee Platnumz”
Kufuatia kauli ya Mobetto ya kudai kwamba yeye ndiye mwanamke pekee anayependwa na mwanamuziki huyo, mashabiki wakasema kwamba inawezekana ameagiziwa ndinga hiyo kwa ajili ya kumpeleka mtoto kliniki.
Loading...
Post a Comment