Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema hayo leo katika kikao chake na baraza la ujenzi, ambapo kimewakutanisha wataalamu wa ujenzi kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuangalia changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo na kuzitafutia ufumbuzi.
"Kwa sasa hakuna taarifa sahihi kuhusu masuala ya ujenzi nchini, sekta ambayo inachangia kwa asilimia 14 ya pato la taifa na haikui kiushindani na nchi zilizoendelea kwa kiwango cha kisasa", amesema Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi nchini, Prof. Mayunga Mkunya amesema hakuna ushirikiano mzuri katika sekta ya ujenzi hali ambayo inachangia kukosa kuwa na mipango endelevu.
Post a Comment