Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Makonda uso kwa uso na akina Mama wa Vingunguti






*MAKONDA WA VINGUNGUTI*

Mamia ya Kina *MAMA* kutoka Eneo la *VINGUNGUTI* majengo wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam _Mhe Paul Makonda_ *MBUZI watatu (3)* kama *ZAWADI* ya Kuunga mkono jitihada anazozifanya katika kupigania Afya ya *MAMA na MTOTO* kwa kuwajengea *WODI* na *VITANDA* vya kina mama watakaolazwa na Watoto.

Wakikabidhi zawadi ya *MBUZI* hao watatu, kina mama hao wamesema Mbali na kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam _Mhe Paul Makonda_ katika masuala ya Afya za Kina mama na watoto, pia *WAMEMPONGEZA* kwa kufanikisha Vita ya *DAWA za Kulevya* ambayo kwa kiasi kikubwaa *ILIWAATHIRI* watoto na vijana wao wengi katika maeneo ya *VINGUNGUTI,* ambao sasa hivi wameanza kupata *UNAFUU* mkubwa kutokana na kupotea kwa Dawa za Kulevya katika maeneo yao.

Mbali na Mbuzi hao, kina Mama wa *VINGUNGUTI* wamesema wataendelea *KUMUOMBEA KWA MUNGU* amsadie Nguvu ya kuendelea kuwatumikia zaidi.

*Taarifa ya Kina Mama Wazalendo kutoka Vingunguti.*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top