Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dereva wa Lissu pasua kichwa ... IGP akomaa nae

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

IGP Sirro akizungumza  Jumatano akiwa ziarani mkoani Mtwara amemtaka dereva wa Lissu kulisaidia jeshi hilo katika kukamilisha upelelezi.

Lissu ambaye anapata matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Alisema miongoni mwa wanaohitajika kwa kuhojiwa ni dereva wa Lissu ambaye inaelezwa yuko Nairobi anakopatiwa matibabu ya kisaikolojia.

“Yule kijana kwenye picha ukimwona yuko vizuri tu, sasa wanaposema anapata huduma ya kisaikolojia wakati kwenye magazeti anaonekana hii inatupa changamoto. Ndugu zangu, mheshimiwa Lissu amepigwa risasi na watu tunaowatafuta, huyo kijana aje. Kuja kwake kutatusaidia kupata majibu ya mambo mengi,” alisema IGP Sirro.

Alisema, “Mtu anasema anatibiwa kisaikolojia lakini kila siku nikiona magazeti anaonekana anawaka, inanipa tabu.”

IGP Sirro aliwataka waandishi wa habari kuwasilisha taarifa hiyo kwa umma akisema, “Kimsingi waandishi wa habari naomba mlipeleke hili sisi tuna uchungu sana na mheshimiwa Tundu Lissu, tunamheshimu ni mtu muhimu kwa Watanzania na sisi tunataka tuwapate waliofanya lile tukio lakini ushirikiano ni mzuri ili  kufanikiwa,” 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top