Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Haijawahi kutokea UVCCM

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umeweka rekodi ya kupokea watu wengi zaidi wakiwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja huo.

Jumla ya wanachama 113 kutoka bara na visiwani wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti Taifa kwenye uchaguzi utakaofanyika mwaka huu. Idadi hiyo inatajwa kuwa haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Hilo limebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamidu ambaye amesema wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM wanafanya usahili wa wagombea waliomba nafasi mbalimbali za uongozi.

Shaka amesema kuwa mchakato huo umeanza tangu mwezi Aprili ambapo tayari viongozi mbalimbali wa ngazi za shina hadi wilaya wamepatikana hivi sasa mchakato unaoendelea ni kuwapata wagombea wa nafasi za kitaifa.

Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi ujao ni Mwenyekiti, na Makamu wake, Wajumbe watano wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa baraza kuu la umoja huo Taifa na wawakilisha wa Jumuiya hiyo katika Jumuiya nyingine ndani ya chama.

Aidha katika nafasi zingine Shaka amesema Vijana 118 wamejitokeza kuwania nafasi ya Ujumbe wa NEC, wakati wengine 23 wakiwania nafasi ya Makamu mwenyekiti. Nafasi ya Mwenyekiti (UVCCM) Taifa inashikiliwa na Mbunge wa Donge Visiwani Zanzibar, Sadifa Juma Khamis aliyechaguliwa mwaka 2012.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top