Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar Mh Ayoub Mahmoud amewashukuru waandishi wa habari kwa kufanya uhamasishaji wa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kilele cha mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na kumbukizi za miaka 18 kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
RC Ayoub amewashukuru vioongozi wote wa kitaifa walioandika historia kwa kuhudhuria kilele hicho cha mbio za Mwenge katika uwanja Amaan visiwani humo.
RC Ayoub amewapongeza wnanchi wote waliojitokeza kwani wametoa hamasa kubwa jambo lililopelekea mgeni rasmi wa shughuli hiyo Rais John Pombe Magufuli kupongeza maandilizi yaliyofanywa kwa ustadi wake na kifanikisha tukio kuhitimishwa salama.
RC Ayoub amewaomba wanahabari na wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kwa maendeleo ya taifa, pia ameyashukuru makampuni mbalimbali kwa kujitolea kufanikisha kilele cha mbio za Mwenge na huduma mbalimbali za kijamii.
Post a Comment