Oktoba 29 miaka 58 iliyopita alizaliwa Mtoto ambaye Leo hii ni Kiongozi mkombozi wa Taifa la Tanzania.
Naam! Namzungumzia Dk. John Pombe Joseph Magufuli (JPM) aliyezaliwa kijijini Chato mikononi mwa Wafugaji na Wakulima lakini kwa jitihada Kubwa binafsi na mapenzi yake Mwenyezi Mungu zimefanya Leo hii tunamwita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Magufuli anasifika zaidi na Watanzania kwa sifa kuu 3 ambazo ni Uchapakazi, Ufuatiliaji na Uzalendo zinazomfanya kuwa miongoni mwa Viongozi wenye historia isiyofutika Tanzania na Kiongozi wa aina yake ya kipekee katika karne hii ya Dunia ya sasa.
Tunakushukuru Rais Magufuli kwa uchapakazi wako wa kuhakikisha unapambana vilivyo na maadui zetu wa kitaifa "ujinga", " maradhi" na " umaskini".
Ahsante sana Dk. Magufuli kwa uzalendo wako uliouonyesha wa kusimamia rasilimali za Taifa ili ziwanufaishe Watanzania wote. Hakika tunaona jitihada za Dk. Magufuli kuleta ukombozi wa kiuchumi nchini Tanzania.
Useme umwongelee Dk. Magufuli na mema yake aliyoyafanya kwa Taifa itakuchukua miezi kwa miezi kumwelezea. Itoshe kusema, Rais Magufuli ni zawadi kwa Watanzania toka kwa Mwenyezi Mungu.
Jukumu letu Watanzania ni kuendelea kumuombea Rais Magufuli katika jitihada anazozifanya kwenye ujenzi wa Taifa letu kufika Tanzania ya Viwanda, kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati.
Magufuli ulizaliwa kwa lengo, Mwenyezi Mungu alikuleta Tanzania kulitimiza. Ahsante sana Mwenyezi Mungu kutuletea Dk. John Joseph Magufuli hapa Tanzania.
Umegusa maisha ya walio wengi, haswa Wanyonge. Umeleta tumaini jipya hapa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla. Sisi Watanzania tunakuombea Dk. Magufuli ujaaliwe maisha Marefu hapa Duniani.
NDIKULOMBELA UHANGAME RAIS WANE DOGTA JOHN POMBE MAGUFULI.
Heri ya Kuzaliwa Rais wetu Mpendwa Dk. John Magufuli.
Mungu Mbariki Rais Dk. MAGUFULI
Mungu Ibariki Tanzania.
Emmanuel J. Shilatu
29/10/2017
0767488622
on Sunday, October 29, 2017
Post a Comment