Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli: Sitafuta mbio za Mwenge


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema hatafuta Mwenge wa Uhuru katika kipindi chake cha uongozi kwasababu una faida mbalimbali kwa taifa.

Hayo ameyasema leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.

Rais Magufuli amesema kwenye awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa Uhuru.

“Nafahamu kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa mbio za Mwenge zimekuwa zikisaidia kubaini madudu mbalimbali yanayofanyika kwenye Halmashauri nchini ikiwemo Miradi hewa. Rais ameahidi kuipitia ripoti nzima ya mbio hizo na kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyoainishwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top