Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Watakao pata vibali vya matibabu nje ya nchi ni wagonjwa wa saratani tu.

Serikali haitatoa tena vibali vya wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa baada ya kuboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa matibabu ya figo isipokuwa wagonjwa wa saratani tena kwa vipimo ambavyo havipatikani nchini.

Katibu mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto Dk Mpoki Ulisubisya ameyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kupokea timu ya wataalamu wakiwemo madaktari bingwa wa fani mbalimbali kutoka nchini Cuba ambapo amesema serikali itakapokamilisha mchakato wa kufunga mashine ambazo kwa sasa hizipo kwa ajili ya wagonjwa wa saratani hakuna mgonjwa yeyote atakayepewa kibali kwenda nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao wameratibu wataalamu hao kuja nchini amesema timu hiyo ina watalaamu 16 na wamelazimika kufanya hivyo baada ya kuboresha maeneo mbalimbali ikiwemo chumba cha watu mahututi ICU ambacho kilikuwa na vitanda 21 kwa sasa kina vitanda 88 changamoto ikabaki kwenye ukosefu wa wataalam.

Baaadhi ya wananchi na waliofika katika hospitali hiyo kupata huduma mbali nakuipongeza serikali wameiomba kutoa kupaumbele kwenye huduma ya mama na mtoto ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top