Baada ya kuapishwa kuwa Waziri wa Maliasili, Dkt Hamis Kigwangala ameweka wazi mipango yake katika wizara hiyo nyeti na kusema kipaumbele chake ni kuhakikisha ujangili unakoma nchini.
Kupitia Mtandao wake wa kijamii Kigwangalla amesema kwamba atafumua mtandao wa majangili na makando kando yake.
"Majangili watawakimbia Tembo kuanzia sasa. Tutahakikisha ujangili unakoma nchini
Aidha ameongeza kwamba "Tutaweka mikakati mipya ya namna ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii. Ni kupitia kujitangaza ndipo tutakuza mapato yanayotokana na utalii. Kazi pia tuliyonayo ni kutatua migogoro ya Loliondo, wafugaji wanaovamia hifadhi n.k.
Mbali na hayo Kigwangalla ameweka wazi hatoacha kuwasemea wanawake. "Sintoacha kuwa Balozi wa wanawake. Nitaendelea kuwasemea na kuwatumikia.
Kigwamngalla amepanda ngazi ya uongozi kutokea kwenye Unaibu Waziri mpaka kuwa Waziri wa Maliasia na Utalii baada ya Rais Magufuli kutangaza mabadiliko ya baraza la mawaziri Jumamosi iliyopita.
Burhan awekewa vikwazo na Marekani
4 hours ago
Post a Comment