Rais Dk. John Magufuli, ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali, kwa tuhuma za kuandika madai yasiyo halali, kwa lengo la kuiibia serikali.
Rais Magufuli ametoa amri hiyo wakati akizindua Uwanja wa Ndege wa Bukoba wenye urefu wa kilomita 1.5 ambapo amewataja watumishi hao kuwa ni Jackson Kaswahili Robert, Mwachano Msingwa na Gidioni Zakayo.
Alifafanua kwamba, Jackson alijaza fomu zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.626 lakini madai hayo yalipochunguzwa, ilibainika kuwa hadai chochote.
Akaongeza kwamba Mwachano yeye alijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.754 wakati ukweli ni kwamba anaidai shilingi milioni 2 tu huku Gidioni Zakayo
Akijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi milioni 104 wakati si kweli.
“Hawa wote pamoja na maofisa wizarani walioidhinisha malipo haya, naagiza vyombo vya dola viwashughulikie. Tumekuwa na watu ambao hawana uchungu na wengine,” alisema Rais Magufuli.
Post a Comment