![Image may contain: 1 person](https://scontent.fnbo1-1.fna.fbcdn.net/v/t1.0-9/22730601_729640470580199_3231586124137641548_n.jpg?_nc_eui2=v1%3AAeGiZpeB9l3s4WS_uPouZng38dunLCTGjKvuTXp13oOqXgUfGD9Vb6gaZDBLtlFKNF-pcvvGnnq02SjFp-nXmrIOkSBEJqjMYoliJeA7d4twzQ&oh=34e3aede02cb8f63e71ca646413c3472&oe=5A92928E)
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema Rais Dk John Pombe Magufuli hajawahi kutamka mahali popote kama Serikali ni ya kwake na si ya CCM kama ilivyodaiwa na kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Aikael Mbowe.
Pia umoja huo umesema pamoja na Serikali kuongozwa na Rais Magufuli bado iko chini ya Chama Cha Mapinduzi na kumtaka Mbowe kuacha maneno ya upotoshaji na uchochezi wa kitoto.
Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozumgumza na waandiahi wa habari ofisini kwake huko Upanga jijini Dar es salaam kufuatia madai ya Mbowe dhidi ya Rais na utawala wake.
Shaka alisema Rais Dk Magufuli tokea alipoingia madarakani miaka miwili iliopita amekuwa akihimiza shime ya kukuza fikra mpya na kudumisha uzalendo ulioporomoka na kuzaa kundi la mafisadi, wezi wa mali za umma bila kujali itikadi za kisiasa kwasababu uzalendo hauna alama ya siasa au chama.
Alisema matamshi ya Mbowe hayana msingi wala mantiki yoyote bali anaonekana kama mtu anayeweweseka usingizini baadaa ya kuona utendaji wa Serikali ya CCM kwa miaka miwili ukiendeshwa kwa uwajibikaji, ufanisi, umakini na kuweka pembeni mitazamo hafifu ya kisiasa huku ikijali zaidi nchi na utaifa.
"Mbowe ni mwanasiasa mnafiki na profesa wa kuzua .Aamesahau alipowakusanya wananchi pale Mwembeyanga Temeke na kutaja orodha ya viongozi wa Serikali aliodai ni mafisadi likiwemo jina la Edward Lowassa aliyehamia Chadema na kuteuliwa kuwa mgombea urais "Alisema Shaka.
Alieleza kuwa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 /2020 ni miliki ya ya CCM na Rais Dk Magufuli hana ilani binafsi ya uchaguzi hivyo akamtaka Mbowe aache kumlisha maneno Rais kwa kusaka kwake umaarufu dhaifu wa kisiasa .
Akizungumzia madai kuwa utawala wa Rais Dk Magufuli umekuwa ni wa kimabavu, ubaguzi na kujali ukanda na ukabila, Shaka alisema huo ni uzushi mpya kwani sera ya ukanda, ukabila na udini ni ya Chadema kutokakana na ushahidi mwingi.
"Mbowe aache kufuatilia mambo ya ccm kwasabahu hayatamsaidia yeye au chama chake. Hana sifa ya kuwa kiongozi mkweli mbele ya watanzania kwasababu ni wakala wa mafisadi na chama chake kimekuwa maficho ya viongozi wasiotamanika katika jamii "Alieleza
Aidha alisema Serikali ya awamu ya tano haijawahi kukataa kupokea ushauri au maoni ndiyo maana Rais Dk Magufuli amekubali hata kupokea ilani ya uchaguzi ya ACT Wazalendo na madai ya kuteua viongozi kwa mtazamo wa udini, ukabila au ukanda huo ni upuuzi usiohitaji kusikilizwa .
Kaimu huyo katibu Mkuu alisema CCM itaendelea kuamini na kufuata itikadi ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ujamaa si utitiri wa vibanda vya nyasi na kadhia ya umasikini bali ni imani na utekelezaji.
Kuhusu ushiriki wa sekta binafsi, Kaimu huyo katibu mkuu alisema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kwa umakini na uangalifu mpya ili kukwepa yaliotokea nyuma yasijirudie tena na kukuta faida au tija ya rasilimali za Taifa zikiwanhfaisha mabepari na mafisadi.
Shaka alisema anachokiamini kwa mujibu wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020, Serikali haijaibeza sekta binafsi, kupuuzia uwekezaji na wawekezaji au kutofungua milango ya ushirika wa maendeleo bali kinachowatatiza baadhi ya mafisadi na wanasiasa uchwara ni kuzibwa kwa mirija na mianya ya wizi wao.
"Kiongozi yeyote anayekuwa wa kwanza kuumwa au kuthubutu kuutaja udini na ukabila hadharani huyo ndiye mkabila na mdini halisi. Hatuwezi kuteua viongozi kwa kutazama idadi ya makabila. ,dini au ukanda kwasababu Serikali si kilenge cha mizimu na matambiko "Alisema .
Pia Umoja wa Vijana umeelezea kusikitishwa kwake na matamshi ya Mbowe kudai hali ya uchumi ni mbaya wakati takwimu za uchumi katika taasisi za kitaifa na kimataifa zikiutaja uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi.
Shaka pia aliyabeza madai ya Mbowe yanayodai huwezi kujenga viwanda ikiwa huna soko huku akisahau kuwa hata yeye alipojenga klab Bllccanas hakuongia mkataba kwa ujio wa wacheza disco au wanywa pombe .
"Huwezi kuwahimiza waumini wa kikristo au waislam kufanya ibada ikiwa hukuna misikiti au makanisa.Tunajenga viwanda , tutazalisha ili kupata masoko ya ndani na nje kutokana na ubora wa bidhaa. Hata Wachina, Waingereza na Wamarekani hatukukubalia kama tutanunua bidhaa zao" Alieleza
Hata hivyo Shaka alisema Rais Magufuli na Seikali inayoongozwa na CCM itaendelea na mikakati yake katika dhamira ya kujenga uchumi imara wa viwanda kuelekea uchumi wa kati , kuziba mifereji ya wizi na ufisadi bila kuyumbiswa na mayowe ya wapinzani.
Post a Comment