Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dk. Magufuli Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa CCM Kwa Kura ZOTE

Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana mpango wa kubadilisha Sekretarieti ya chama hicho na itaendelea kama ilivyo chini ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.

Mwenyekiti huyo mpya alichaguliwa kwenye mkutano wa tisa wa chama hicho uliomalizika jana jioni mjini Dodoma kwa kupata kura zote 1821 za wajumbe wa mkutano mkuu. 

Rais Magufuli atahudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano kuanzia jana hadi mwaka 2022 utakapofanyika uchaguzi mwingine.

Katika hotuba yake baada ya kuchaguliwa Dkt. Magufuli alisema kwasasa hana mpango wa kubadilisha Sekretarieti na itaendelea kama ilivyo chini ya katibu mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana.

Matokeo ya Uchaguzi huo yalitangazwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ambaye aliwataja washindi wote katika nafasi za Mwenyekiti Taifa, Mwenyekiti Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Taifa.

Mbali na Mwenyekiti wa Taifa lakini pia Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura zote 1821 wakati Ndugu Philip Mangula akishinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Taifa kwa kura zote 1821.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top