Loading...
Dk. Magufuli apasua jipu UWT
*NUKUU ZA MWENYEKITI WA CCM NDG. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWENYE UFUNGUZI WA KIKAO CHA UWT TAIFA*
Desemba 08, 2017.
Dodoma.
1. " Tunataka kuwa na wanachama na viongozi waliopatikana kwa halali, hii nazungumza kwa Chama chote iwe wazazi, UWT ama vijana " - JPM
2. "Kama tumeamua kupingana na rushwa kwenye serikali Lazima tupingane na Rushwa na kwenye chama".- JPM
3. "Mtakavyo kuwa mnachagua leo msiangalie amekupa kiasi gani, amekulipia hoteli kiasi gani, chagueni kiongozi anaye amini kanuni na katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)". JPM
4. "Nataka mchague kiongozi atakaye waweka pamoja wakina mama" JPM
5. "Nasema kwa dhati nawapenda sana wakina mama, naomba mnisaidie yule mtakaye mchagua awe kila siku mtetezi wa wakina mama" JPM
6. "Atambue kiongozi siyo mfalme kiongozi ni kuwatumikia unaowaongoza"JPM
7. "Kiongozi wa UWT ngazi ya taifa siyo jukumu dogo ni jukumu kubwa, jumuia hii ni muhimu sana kwa Chama chetu cha Mapinduzi" JPM
8. "Naomba Ndugu zangu mchague kwa umakini mkubwa siyo kwa ukanda, udini, ukabila na Kamwe msichague mtoa rushwa tukumbuke ahadi namba 3 ya mwanaCCM" JPM
9. "Chama chetu kimefanya mageuzi makubwa na tumelenga kukifanya kuwa chama cha wanachama hivyo UWT lazima iwe ya wanawake wote siyo ya mtu mmoja " JPM
10. "Benki ya wanawake haifanyi vizuri Tangu ianzishwe utendaji kazi wake hairidhishi" JPM
11." Na wakopaji wengi pale ni wanaume na inariba kubwa kweli kwa wanawake". JPM
12. "Tunaipitia vizuri ili benki ya wanawake iwe kwa uhalisia kimbilio la wanawake hasa wale walio pembezoni" JPM
13. "Niwaombe uongozi huu mpya mnaouchagua mkafanye mageuzi kwenye benki ile ya wanawake maana inawanyonya wanawake".JPM
14. "Mimi ninadeni kubwa la kuwatumikia ila ninyi mnadeni kubwa zaidi leo la kuchagua viongozi wanaoweza kuenda na muelekeo wangu" JPM
Imetolewa na:
Idara ya Itikadi na Uenezi
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Post a Comment