Loading...
Kheri James aeleza UVCCM anayoitaka
*YALIYOSEMWA NA MWENYEKITI UVCCM KHERI JAMES KWENYE MAPOKEZI MKOA WA DAR ES SALAAM NDANI YA UKUMBI WA VIJANA SOCIAL HALL DISEMBA 21, 2017*
"Nataka tuwe na jumuiya ambayo ni kimbilio LA Vijana wote" - Kheri James
"Habari ya kuwa na Vijana ambao viongozi wao wanapenda kupigiwa makofi, kiongozi ambao ni mlevi, muhuni na unachafua taswira ya Vijana tutakufukuza" - Kheri James
"Viongozi wa Serikali ambao watakuwa na dharau kwa Vijana hawa hatutawavumilia" - Kheri James
"Viongozi wa Serikali wanapokea tusiwaonee haya kuwaambia wanakosea hadharani" - Kheri James
"Kama kuna jambo lina furahisha ama linakera tuwaachie wenye dhamana yao waseme. Sitaki kusikia anayejiita kada wa CCM wanasema sema ovyo mitaani kwa ngazi ya Taifa" - Kheri James
"Rufaa zote zilizoletwa na kuthibitika rushwa imetumika tutafuta ushindi wao" - Kheri James
"Nataka kila kiongozi mwenye uwezo wa kiuongozi agombee pasipo kujali uwezo wake wa kifedha" - Kheri James
"Nataka uhakiki uendelee mapema kabla tume ya Rais Dk. Magufuli kuja kuhakiki" - Kheri James
Nimewateua Sophia Kizigo, Ndugu Manumba na Ndugu Saitoti pamoja na wajumbe wengine watakao tangazwa na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka kuongoza timu ya kuhakiki Mali za jumuiya" - Shaka
"Nataka wakati wa zoezi LA uhakiki linapokuja kwenye eneo, timu niliyoiunda ipewe documents ama wapelekwe site na si blah blah tu" - Kheri James
"Nataka viongozi wote waanzishe miradi mipya na si kuangalia Mali tulizopo pia" - Kheri James
"Tabia, khulka na mienendo ya Rais Magufuli imesaidia kuongeza imani kwa CCM, nataka hali hii ihamie kwa viongozi wa UVCCM" - Kheri James
"Viongozi wote tuwe chachu ya kuwaonyesha njia ya mafanikio kwa Vijana" - Kheri James
"Nataka vibaraka, wahujumu Mali za jumuiya wasakwe na watimuliwe" - Kheri James
"Tunataka pesa za Manispaa zile za asilimia 5 za Vijana zitoe pesa hizi na wala hatuwaombi. Wakishindwa kutoa tupeni taarifa" - Kheri James
"Wanaojua Mali za Jumuiya ambazo hazionekani, viwanja vimeuzwa na unavijua njoo ofisini uniambie Nina kifua nitakulinda" - Kheri James
"Wilaya yangu ya Ilemela ndio wilaya ya mfano kutoa asilimia 5 kwa Vijana kipindi nilichokuwa Mwenyekiti UVCCM Wilaya" - Kheri James
"Ni aibu kijana anayekipigania chama kutetewa na kujaliwa nyakati zote" - Kheri James
"Uchaguzi umekwisha. Tuache kuendelea na masuala ya uchaguzi" - Kheri James
"Dar es Salaam iwe mfano ya ushindi kwenye chaguzi za Kiserikali, nataka ushindi tu" - Kheri James
"Hatutolipa visasi, hatutamuonea mtu bali tutashirikiane na kila mtu kuijenga jumuiya yetu. Mliopata nafasi, msilipe visasi" - Kheri James
"Nawaletea salaam toka kwa Dk. Magufuli anawapenda sana. Amewaomba muelezee mema ya Serikali" - Kheri James
"Kazi kubwa inafanyika. Shindaneni kuelezea mema ya Serikali iliyopo madarakani" - Kheri James
Kheri James ni Mwenyekiti UVCCM Taifa aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye mapokezi yake katika ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam Alhamis Disemba 21, 2017
Imeandaliwa Na:
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Post a Comment