Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Novemba mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 4.4 ikilinganishwa na asilimia 5.1 iliyokuwa mwezi Oktoba.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa Kwa mara nyingine nasema mfumuko wa bei umefikia asilimia 4.4.
Aidha amesema kuwa kupungua kwa Mfumuko wa bei mwezi Novemba mwaka huu kumechangiwa hasa kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Novemba mwaka huu zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba mwaka jana.
Hata hivyo alisema kuwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na nyama ya ngo’mbe kwa asilimia 5.4, samaki wabichi kwa asilimia 22.2, mbogamboga kwa asilimia 3.9, viazi mviringo kwa asilimia 14.0, mihogo mibichi kwa asilimia 24.8 na viazi vitamu kwa asilimia 13.4.
Trump ahutubia wafuasi wake Jumapili mjini Washington
42 minutes ago
Post a Comment