Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi, Julius Kawondo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni
Jafo amewaambia waandishi wa habari leo Ijumaa kuwa Kawondo ameshindwa kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.
"Natumia Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na Sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo," amesema Jafo.
Amesema fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa Kijiji cha Kamwanda ambako mkurugenzi alishirikiana na mmoja wa maofisa kutoka wizara ya maji.
Jafo amemuomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi huyo kuhujumu mradi wa maji katika Kijiji cha Kamwanda wilayani humo.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
Rinazon Ministry Ukombozi kwa Wanandoa16 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment