Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe mapema leo amekagua mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika jimbo la Nzega Mjini.
Tayari mkandarasi ameanza ujenzi wa matanki makubwa ya maji na njia za kupitisha mabomba makubwa ambayo yataifanya Nzega Mjini kuwa kitovu kikuu cha Usambazaji wa Maji haya ya Ziwa Victoria.
Katika kuhakikisha mradi huu unanufaisha wananchi wote wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Bashe aliwasilisha maombi binafsi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli fedha kwa ajili ya kupanua mtandao wa Maji Nzega na tayari Rais amekwisha kutoa fedha hizo ili kuboresha upatikanaji wa Maji ya uhakika katika Mji wa Nzega ambao kwa miaka mingi umekua na kilio kikubwa.
Kwa upande mwingine Mhe. Bashe ametembelea eneo la Sagara ambapo kwa pamoja na Halmashauri ya Mji wa Nzega wamekusudia kujenga kisima kikubwa chenye uwezo wa kusambaza maji kwenye maeneo jirani. Upanuzi wa kisima hiki ni katika juhudi mahsusi za kuhakikisha hakuna tena tatizo la maji Nzega.
Aidha, kuhusiana na ajira zitakazotokana na mradi huu Mhe. Bashe amesema "Kipaumbele kwa ajira ambazo zitatokana na mradi huu watapewa watanzania ambao wanaoishi katika maeneo ambayo mradi unapita ili kuhakikisha mzunguko wa fedha na ajira zinakuwepo kwa vijana na wananchi ndani ya Mji wa Nzega"
Post a Comment