Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja.
Na Athumani Shariff- MoWI
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo amezindua miradi miwili ya maji ambayo ipo Halmashauri za Wilaya ya Mtwara na Masasi Mkoani Mtwara ilyogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,764,376,293.19 yote kwa pamoja.
Mradi wa maji wa Mayaya katika Halmashauri ya Mtwara uligharimu shilingi 973,022,925 una vituo 37 vya kuchotea maji na unanufaisha wananchi wapatao 4,997.
Katika Halmashauri ya Masasi Waziri Kamwelwe alizindua mradi wa maji wa Shaurimoyo– Mpindimbi wenye thamani ya shilingi 1,791,353,368.19 ambao utanufaisha wakati wapatao 8,400 washio katika vijiji vya Shaurimoyo, Kachepa, Mpindimbi na Kanyimbi.
Wakati wa uzinduzi wa Miradi hiyo, wananchi walishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwani walikuwa na adha kubwa ya maji ambapo kabla ya mradi walikuwa wakinunua ndoo moja ya lita 20 kwa shilingi elfu moja na baada ya mradi wananunua ndoo moja kwa shilingi hamsini tu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lulindi Jerome Bwanausi amemshukuru Wazira wa Maji na Umwagiliaji na serikali ya awamu ya tano kwa kukamilisha ahadi zao, na ana furaha isiyo na kifani kwa kukamilika miradi hiyo ambayo imeondoa kero kubwa ya maji kwa wananchi.
Waziri Kamwelwe kesho ataendelea na ziara ya kikazi Mkoani Lindi ambapo atakagua mradi wa maji wa Ng’apa kisha ataelekea Wilayani Newala Mkoani Mtwara kwa ajili ya uzinduzi mradi wa maji wa Mapili uliojengwa kwa thamani ya shilingi 1,668,826,940.
Baada ya kukamilika kwa ziara hiyo Mhandisi Kamwelwe atarudi Dodoma alhamisi kuendelea na shughuli za bunge.
Post a Comment