Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James (Kulia) akieleza umuhimu wa wakazi wa Kata ya Kimandolu kumchagua Ndg Gaudence Limona kuwa diwani wao wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018.
Kikao kikiendelea
Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa
Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote
wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa
Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Arusha
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg
Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika
uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila
kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema
hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za
uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za
CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa
Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.
Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na
Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa
wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya
uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo
kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia
aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa
CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa
ujumla wake.
Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya
Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa
Jiji la Arusha.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya
upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na
ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao
haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.
Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa
kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi
madhubuti sio viongozi biskuti.
Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti
wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo
itakuwa zawadi pekee kwake.
“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa
vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi
kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM
ishinde” Alikaririwa Kheri
MWISHO
Post a Comment