Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akimnadi mgombea Udiwani Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo kwenye mkutano wa hadhara wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Ndg Kheri Denice James akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018.
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara za ufungaji wa kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha, Leo 12 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Arusha
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema kuwa nchini Tanzania hakuna Chama chenye uwezo wa kushindana na CCM kwani vyama vilivyopo ni mfano wa kamati za harusi zenye jukumu la kupanga na kuratibu sherehe za ndoa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg Kheri Denice James wakati akifunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Kimandolu Wilaya na Mkoa wa Arusha unaotarajiwa kufanyika kesho 13 Januari 2018.
Kheri amebainisha kuwa pamoja na wananchi kufanya maamuzi ya ama kuchagua jiwe au mtu mwaka 2015 Arusha walipata hasara kubwa kwani matatizo yao yalikosa mtu wa kuyasemea bungeni katika kipindi cha takribani miaka saba sasa.
Alisema kuwa wananchi Mkoani Arusha walifanya makosa Octoba 25, 2018 katika uchaguzi Mkuu kwa kuchagua wawakilisha wa Ubunge na Udiwani wasiokuwa na mtazamo wa kuwasaidia badala yake kujinufaisha wao pekee pasina kujali umuhimu na maslahi makubwa ya wananchi na watanzania waliowachagua.
Alisema kuwa katika kipindi kirefu serikali ya Chama Cha Mapinduzi imekuwa ikizalilishwa na kutukanwa na watanzania waoishi ndani na nje ya nchi lakini imekuwa na uvumilivu mkubwa kwa ajili ya maslahi ya watukanaji na wananchi wote kwa ujumla wake.
Aliongeza kuwa Tanzania katika kipindi hiki imepata Rais anayewapenda na kuwajali wananchi wanyonge ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli aliyeleta heshima kubwa kwa kila mwananchi kutokana na maamuzi yake ya kutaka watanzania wote wanufaike na kufaidi matunda ya rasilimali zao.
Aidha, Alisema kuwa katika kipindi kifupu tangu kuteuliwa kwa Mhe Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ubabaishaji umekwisha Mkoani humo kwani wananchi wametambua uduni wa busara kwa viongozi waliowachagua wanaotokana na vyama vya upinzani.
Alisema Mhe Gambo amekuwa ni kijana mzalendo na alama bora katika Taifa hivyo mwananchi wanapaswa kumuunga mkono katika utendaji wake kwani kazi ya uongozi ni kazi kubwa na ngumu sana endapo kama kuna watu watakukwamisha kwa makusudi.
Sambamba na hayo pia Mwenyekiti Kheri alimnadi Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo na kumtaka mara baada ya kuchaguliwa anapaswa kuhakikisha anaboresha huduma za afya, elimu, na miundombinu haraka iwezekanavyo katika Kata hivyo kwa mujibu wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
Post a Comment