Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limemkamata Deogratius Kisandu ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkolani kwa makosa ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kuandika matusi.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutumia ukurasa wake wa Facebook kuandika matusi mazito kwa takriban wiki nzima.
Kisandu ambaye ni kada wa Chadema ameendelea kuweka rekodi ya makada wa Chadema wanaokamatwa kutokana na kutumia vibaya mitandao ya kijamii. Wengineo ni Yericko Nyerere, Bob Chacha Wangwe.
Hata kukamatwa kwa Kisandu bado wana Chadema wameendelea kuudanganya umma kwa kusema Kisandu ni Mwana CCM aliyerubuniwa kwa kununuliwa. Lahaula!
Katika andiko wanalo sambaza wanadai Kisandu alikuwa Chadema baadae akahamia NCCR Mageuzi. Cha kushangaza Chadema hawajasema dau alilolipwa Kisandu kutoka Chadema kwenda NCCR Mageuzi ilikuwa kiasi gani? Kipi kilichomwondoa Chadema?
Kama hakulipwa chochote kuhamia NCCR Mageuzi kwanini akihamia CCM tuaminishwe alihaidiwa malipo ya pesa?
Chadema iache hoja dhaifu! Ukweli unabaki pale pale Kisandu ni Mwana Chadema; Ukweli unabaki pale pale CCM haijawahi kumnunua Kisandu na haijawahi kumnnunua Mtu yeyote yule kama gia ya kumshawishi ajiunge na CCM.
"Kununuliwa" ni hoja dhaifu sana inayotajwa na Chadema na wapinzani wengineo kuaminisha umma kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa ila wanaojiunga na Chadema kuwa ni Makamanda!
Tuache fikra Mfu Chadema ijipange kwa kuacha mienendo ya hovyo mitandaoni kwa kupunguza matusi na kuongeza ushawishi wa hoja. Itumie uweledi katika kukijenga chama chao.
Chadema ijitathmini kwanini kila siku inakimbiwa na Makamanda wake na si kuishia kwa kihoja chepesi eti wananunuliwa.
Haiwezekani CCM inunue Wenyeviti wa Mitaa, Madiwani, Wabunge, inunue mpaka Wanachama wa upinzani?
CCM hainunui Watu hata siku moja. CCM ni kama Maji usipoyaoga, utayapikia ama utayanywa. Hakuna namna ya kukwepa ama kuzuia Watu kukipenda, kukishabikia ama kujiunga nacho.
Ukiikwepa CCM kwenye muundo wake basi utavutiwa na sera zake; Ama ukiikwepa kwenye aina ya siasa zake za kistaarabu basi utavutiwa na utekelezaji wake wa ilani ya uchaguzi. Hiyo ndio CCM!!
*Na Shilatu E.J*
Januari 25, 2018
Januari 25, 2018
Post a Comment