Watu aina ya Salum Mwalimu hawafai wana Kinondoni kutokana na vigezo mbalimbali vinavyompotezea sifa ya kuwa Mwakilishi wa wana Kinondoni.
Ili Kinondoni iweze kubadilika na kupata maendeleo zaidi inamuhitaji Mtu sahihi anayeishi nao na kuzijua shida, kero, matatizo na karaha zao na si kitendo hiki cha aibu na dharau kilichofanywa na Chadema cha kuokoteza Mtu toka mfukoni na kuwaletea wana Kinondoni. Kwani hakuna mwana Kinondoni ambaye angeweza kugombea ubunge mpaka waletewe "wakuja"? Tangu lini Mtu wa Kikwajuni akazijua shida za Watu wa Kinondoni? Hili wana Kinondoni wanalijua vyema na hawapo tayari kupotezewa muda na "wakuja".
Salum Mwalim ambaye 2015 aligombea Ubunge jimbo la Kikwajuni Zanzibar na kuangushwa vibaya vibaya, leo hii kajitosa Bara kugombea ubunge. Ni lazima wana Kinondoni wajiulize kipi kimemfanya akimbie kwao na kukurupuka kwenda ugenini Kinondoni kugombea ubunge? Katika kuonyesha Salum hafai, nyumbani kwao tu walimkataa kwa kumnyima kura 2015. Kama ameshindwa kukubalika kwao, ugenini nani atamthamini?
Salum Mwalim ambaye ameonyesha toka mwanzo ana makando kando mengi tena ya dhahiri ya kubebwa na kundi la makao makuu ya Chadema, ni dhahiri atakao waabudu na kuwasujudia zaidi ni wale wachache waliomfikisha kugombea kuliko Watu wengi wa wana Kinondoni. Sampuli hii ya Watu wa makando kando tumeshawaona sana wanavyoleta majuto kwa jamii. Wana Kinondoni wanalijua hili ndio maana wameonekana mapema kugoma kugeuzwa ngazi.
Salum Mwalim huyu huyu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ameshindwa kabisa kutimiza majukumu yake ya kiutendaji Zanzibar na kuifanya Chadema kuwa chama kisichojulikana wala hakipo 5 bora ya vyama vya Zanzibar. Huu ni ushahidi tosha wa uwezo mdogo wa kiutendaji na kiuongozi aliobarikiwa Salum Mwalim usio na tija kwa wana Kinondoni, na wanalijua hili!
Mapema kabisa wana Kinondoni wamesema hapana kwa upinzani na kuamua kumpata kiunganishi sahihi na Rais wa nchi Dk. Magufuli. Wana Kinondoni wanahitaji maendeleo zaidi ambayo watayapata kwa mgombea wa CCM, Maulid Mtulia
*Na Shilatu E.J*
Januari 24, 2018
Januari 24, 2018
Post a Comment