Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WASHAURI CCM KIRUMBA KUWA ABDURAHMAN KINANA STADIUM

 Image may contain: 4 people, people smiling, people standing

 *Rais Mstaafu atamani Kinana angeendelea kidogo, atuma pongezi nzito;*

 *Akiri Kinana Aliiokoa CCM katika Majaribu makubwa yasiyomithilika;*

 *Alihuisha Mfumo Madhubuti wa Kusikiliza Kero Tangu Mashinani.*

Na Mwandishi Maalum, Dar Es Salaam

27-6-2018: *PONGEZI zimeendelea kumiminika kwa Katibu Mkuu mstaafu wa*
*Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali (mstaafu) Abdulahman Kinana kwa*
*mchango usiomithilika katika kuiimarisha CCM.*

Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu na familia ya Komredi Kinana, alisema kwa ahadi ya kutotajwa kuwa
miongoni mwa walioguswa sana na utendaji wake ni pamoja na Mwenyekiti
Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu, Mhe Benjamin William Mkapa ambaye alilazimika
kumtumia salamu rasmi za pongezi.

Amesema Rais huyo mstaafu alimtumia salamu hizo zilizobeba hisia nzito sana
zilizomtoa machozi ya furaha Komredi Kinana, ambaye anaelezwa kutoa mchango
mkubwa kwa CCM, hasa katika kuasisi mikakati ya ushindi wa chaguzi
mbalimbali tangu 1995 hadi 2015.

“Weledi, ustadi na umahiri vilipambanua dhahiri utendaji wako chamani hasa
kwenye kipindi ambacho chama kilikuwa kinapita katika majaribu makubwa sana
pengine yasiyomithilika tangu kuanzishwa,” amesema mtoa habari wetu akikariri
salamu hizo.

Mtoa habari huyo alieleza kuwa salamu za Rais Mstaafu Mkapa pamoja na zile za
wabunge ambao pia walimkabidha zawadi ya gari, zilikuwa ni faraja kubwa kwa
Komredi Kinana na anayeelezwa kujawa na bashasha kwa utambuzi huo.

“Mathalan, sote tumeshuhudia ushupavu na uthabiti wako kwenye mchakato wa
kuteua wagombea wa urais kupitia chama chetu kwenye uchaguzi uliopita ambapo
uwepo wa makundi kinzani uliteteresha chama na kutishia kuathiri umoja na
mustakabali wa chama,” alisema mtonyaji wetu na kuomba asitajwe kwenye media.
Aidha, mimi binafsi na hata chana chetu kitakukumbuka kwa, pamoja na mambo
mengine, juhudi zako za kukiimarisha chama ambacho ni dhahiri kilikuwa
kinaanza kupoteza umaarufu sehemu za mashinani,” salamu hizo zilisema na
kuongeza kuwa Komredi Kinana alidhibiti hali hiyo kwa kuweka mfumo dhabiti wa kusikiliza na kutatua kero za wanachama.

“Ziara zako za nchi nzima kwa minajiri ya kukutana na na kuzungumza na
wanachama, kusikiliza na kutatua kero zao zilikuwa zenye tija na ni kielelezo tosha cha uongozi wako wa vitendo, mapenzi yako kwa chama chako na nia yako thabiti
ya kukiimarisha zaidi kuhakikisha kinaendelea kushikilia dola ambalo ndilo lengo kuu la kila chama chochote cha siasa,” alizikariri salamu hizo.

Mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM aliyeongoza kwa kauli mbiu ya zama za
ukweli na uwazi, alisema, “Uthabiti wa chama chetu ulioshuhudiwa baada ya ziara
zako zile, itabaki kuwa ni miongoni mwa vielelezo visivyofutika vya michango
mikubwa uliyoitoa kwenye kuhuisha chama na utakumbukwa kwayo.”

“Komredi, ni kutokana na umahiri huu dhahiri, mapenzi yako dhabiti, maono yako
kama kiongozi na pia utumishi wako uliotukuka kwa chama; taarifa za kustaafu kwako zilinitia simanzi, pengine nikitamani uendelee japo kidogo,” alisema mtoa
habari wetu
Alimaliza kwa kumtaka Komredi Kinana kuwa kuendelea kuwa kada hai ili chama
kiendelee kuchota busara zake.

Wananchi mbalimbali waliohojiwa walisema Komredi Kinana ndiye aliyesimamia
na kuongoza ushindi uliomwingiza Bw Mkapa katika Urais mwaka 1995, Jakaya
Kikwete 2005 na Dk John Magufuli 2015.

“Ameiacha CCM ikiwa imara. Ameimarisha mahusiano ya CCM na vyama
vingine vya ukombozi vya Afrika na pia vyama rafiki duniani huku akiitanabaisha
CCM kama kimbilio la wanyonge,” alisema Wilfred Gamba.

Kinana ambaye ni Kanali mstaafu wa jeshi la wananchi anaelezwa kuwa ni jasiri
asiyekubali kushindwa, asiye na visasi na hueshimika kwa wakubwa na wadogo.
“Napendekeza CCM ingempa hadhi anayostahili kwa kuuita uwanja wa CCM
Kirumba kuwa uwanja wa Abdulrahman Kinana. Kwa miongo mitatu, Kinana
ameipigania CCM na kuhakikisha kinashika dola, anastahili hadhi hiyo,” alisema.
Bw Gamba aliongeza kuwa, kwavile Komredi Kinana anaheshimiwa na wabunge
wa itikadi zote za siasa, chochote cha kumbukumbu yake kitaafikiwa hata na
wabunge wote.

Pamoja na kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Komrade Kinana alipata kuwa Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (1985-1990), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (1990-1991) na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (1985-1990).
Kinana pia alipata kuwa Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA),
(2001-2006) na Mbunge wa Arusha kwa vipindi viwili (1985-1995).
Vilevile Komrade Kinana amepata kuwa Mwenyekiti Bodi za taasisi na mashirika
mbalimbali.

Komredi Kinana pia amepata kuwa Mwenyekiti wa Hospitali na Taifa ya Tanzania
tangu mwaka 2001, Mwenyeki wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (2009-2010)
na Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu (2009-2010) na pia
Mwenyekiti wa Bodi wa taasisi mbalimbali za binafsi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top