Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli 'aukomalia' mkataba wa Lugumi


Rais John Magufuli amemuagiza waziri mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kufanya uchunguzi wa mradi wa Sh37 billioni wa ujenzi wa vituo 108 vya polisi ulioingiwa kati ya wizara hiyo na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited.

Amesema Serikali ilipewa maagizo na Bunge kuchukua hatua kwa baadhi wa watu waliobainika kufanya makosa katika utekelezaji wa mradi huo lakini anashangaa mpaka sasa haoni hatua zinazoonekana zikichukuliwa.

Kiongozi Mkuu huyo wa ncuhi ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 2, 2018 Ikulu Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua jana, wakiwemo mawaziri watatu na naibu mawaziri wawili.

“Kuna baadhi ya vitu katika mradi huo havijakamilika, vitu vingine wame-exaggerate (wameongeza makadirio) lakini hakuna hatua zilizochukuliwa,” amesema Rais Magufuli.

Amemwagiza pia kuchukua hatua kwa waliohusika na mradi wa kuagiza magari 777 ya polisi aliyodai yaliagizwa kupitia mkataba wa ovyo.

Amesema baadhi ya magari hayo yaliagizwa kama mapya lakini tayari yametembea zaidi ya kilomita 4, 000 na yapo ambayo hayajaandikwa hata tarehe ya kutengenezwa.

“Mkataba wenyewe ni wa ajabu, nimempeleke katibu mkuu (Wizara ya Mambo ya Ndani) Meja Jenerali sikufanya makosa, nimefanya kwa makusudi. Ninaposema mkataba ni wa ovyo najua ni wa ovyo. Niliowapeleka pale hawakuyaona haya,” amesema Rais Magufuli.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top