Msanii aliyekuja juu
kwa kasi kwa muziki na pia matangazo ya biashara likiwemo la Airtel Money la
kampuni ya simu ya Airtel aliyejulikana kwa jina la Sharobaro a.k.a Sharo Milionea
amefariki dunia leo.
Kamanda wa Polisi
mkoani Tanga, Afande Constatine Masawe, amethibitisha kutokea kwa
kifo cha wa Sharobaro, kufuatia ajali ya gari katika
kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga ambako ndio nyumbani kwao.
KWA MUJIBU WA WASANII
WENZAKE AMBAO NI MWANADADA SHILOLE NA STEVE NYERERE (KWA WAKATI
TOFAUTI),WAMETHIBIBISHA KUTOKEA KWA AJALI HIYO NA KUSEMA KUWA MSANII MWENZAO
HUYO,AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA AJALI HIYO,JIONI YA LEO.
Habari zaidi zitakuja kadri zitavyotufikia.
Globu ya Jamii imepokea habari hizi kwa mstuko na masikitiko
makubwa kwani nyota ya Sharo Milionea ndiyo ilikuwa inaanza kung'ara katika
anga za muziki pamoja na matangazo ya biashara, akiwa kayapumulia pumzi mpya wa
ubunifu na weledi katika kupeleka ujumbe kwa watazamaji ambao wakubwa na wadogo
walimpenda.
Mola aiweke roho ya marehemu
mahali pema peponi - Amina
............................ Endelea kufuatilia NDGSHILATU BLOG nitakujuza zaidi ............
on Monday, November 26, 2012
1 comments:
kwa kweli mimi ni mama ambaye si mshabiki sana na mambo ya miziki lakini kijana huyu ameniuma sana tena sana, na nimeanza kumfahamu kipindi kifupi sana hasa kwa kupitia matangazo ya Airtel na Azam kabla ya hapo sikuwa namjua kabisa. Mungu amlaze mahali pema peponi Amin.
ReplyPost a Comment