Brass Band
ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake
yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi
wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Maandanamo
yakipokelewa na Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya
Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora
Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na
Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula,Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema (pili kulia) pamoja na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyera.
Balozi wa
Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye basi aina
ya Toyota Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa Wildaf
wanaokwenda Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa
Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya
Wanawake.
Mgeni rasmi katika Mkutano
huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akisoma
Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf waliohudhulia Mkutano huo leo
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Wengine
Pichani toka kulia ni,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said
Mwema,Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo
ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula na Mkurugenzi wa Mambo ya
Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora
Msechu.
Mwenyekiti
wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi
Kaihula akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Ukaribisho katika Mkutano wa
Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya
Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.
Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya aina
mpya ya Karatasi maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na tatizo la
Majeraha (PF 3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi ya Vipengele
Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya
Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Post a Comment