MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO,
JOHN MNYIKA.
MBUNGE wa Jimbo la
Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema licha ya kuwa na orodha ya vigogo
walioficha fedha Uswiss, lakini hawezi kutoa orodha ya majina hayo kama Serikali
inavyotaka kwa vile orodha ya vinara wa ufisadi ambayo ilitajwa Mwembe Yanga
bado haijashughulikiwa.
Akizungumza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sahara jijini Mwanza, Mnyika
alisema kwamba kama Serikali ya CCM inasisitiza kutaka majina ya walioficha
fedha huko Uswiss yatajwe, wanapaswa kusimama na kueleza ile orodha ya mafisadi
ambayo Chadema waliitaja pale Mwembe Yanga imefanyiwa kazi
gani.
“Watu wanapotutaka
tutaje majina, na sisi tunawambia kwanza wasimame na kutueleza ile ‘list’
(orodha) ya mafisadi ambayo tuliitaja kwa majina wameishughulikia vipi
?”.
Alihoji Mnyika na
kuongeza kwamba wanajua jinsi ambavyo CCM wanalivyonufaika na ufisadi kupitia
Kampuni ya Kagoda jambo ambalo linadhihirisha kuwa haiwezi kuwa rahisi kwao
kushughulika na vita ya ufisadi.
Alisisitiza kuwa
wanaotaka majina yatajwe wanayo ajenda yao na wao wameshaifahamu hivyo
hawatashughulika nayo na kusema ukifika wakati ambao wao wanautambua wataweka
kila kitu nje, lakini siyo kwa kushinikizwa na Serikali ya
CCM.
“Tunajua serikali hii
inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi haina dhamira ya kushughulika na ufisadi, na
hili ndilo litakalowaondoa madarakani,” alifafanua.
Hata hivyo mkutano huo
uliingia dosari wakati Mnyika akiendelea kuhutubia ambapo mawe yalianza kurushwa
na vijana wanaodaiwa kuwa ni vijana wa Diwani wa Kata ya Kitangiri kwa tiketi ya
Chadema, Henry Matata aliyevuliwa uanachama.
Kutokana hali hiyo
vijana wa Chadema walizungumza katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwanasa
vijana wawili ambao walishambuliwa na kueleza na kunusuriwa na Mbunge wa
Nyamagana Ezekiel Wenje aliyeita polisi na kuwaomba waache
kuwashambulia.
Awali akizungumza katika
mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Wenje alieleza wananchi kuwa katika
mkakati wake wa kuboresha elimu ya msingi na sekondari amefanikiwa kutengeneza
madawati mengine 400 baada ya madawati ya awali 500 kugawiwa katika
shule.
Alisema madawati hayo
yatagawanywa kwa shule 30 za wilaya ya Nyamagana na kubainisha kwamba kutokana
na madaati ya awali 500 kutolewa bila utaratibu na Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza,Wilson Kabwe hivyo madawati haya alieleza kuwa yatasambazwa na madiwani
wa Chadema katika shule pamoja na katibu wa ofisi yake ili kuhakikisha yanafika
katika shule husika iliyopangwa.
Post a Comment