Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa mpira, mjini
Geita mkoani Geita, jioni hii, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya mikoa
minne kujitambulisha kwa wanachama na kukagua uhai wa chama ngazi za mashina na
matawi na kusimamia na kueleza utekelezaji wa ilani ya
Chama.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi
leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu, Geita, katika mkutano wa hadhara
uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni 21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji
hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha wachimbaji wadogo nao kunufaika
na madini badala ya wachimbaji wakubwa tu.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
akizindua shina la wakereketwa wa CCM la wajasiriamali watengeneza fenicha
katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, leo. Nape aliwapa pia ,msaada wa sh.
milioni moja kwa ajili ya wajasiriamali hao kukuza shughuli
zao.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akikabidhi leseni za wachimbaji wadogo machimbo ya Mugusu,
Geita, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo mkoani Geita. Jumla ya leseni
21 zilikabidhiwa kwa wachimbaji hao baada ya kutolewa na serikali ili kuwwezesha
wachimbaji wadogo nao kunufaika na m,adini badala ya wachimbaji wakubwa
tu.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye,
akisalimiana na vijana wa mji wa Katoro wanaojishughulisha na biashara
ndogo.







Post a Comment