Wafuasi na wapinzani wa rais wa Misri Mohamed Morsi wameitisha maandamano makubwa leo Ijumaa baada ya kiongozi huyo kujipa madaraka makubwa ambayo wachambuzi wansema kuwa yanamfanya kuwa dikteta.
Safu ya vikundi huria na
visivyo na mlengo, ikiwa ni pamoja na wanaharakati waliokuwa mstari wa mbele
katika harakati zilizomwondosha madarakani kiongozi mkongwe wa taifa
hilo.
Hosni Mubarak mapema
mwaka jana, wamepanga kufanya maandamano katika bustani ya Tahrir jijini Cairo,
eneo ambalo ni kitovu cha maandamano, kupinga hatua ya kiongozi huyo ambaye
amebatizwa jina la farao mpya.
Wafuasi wa Morsi
wakiongozwa na chama chenye nguvu cha Muslim Brotherhood wamekusanyika nje ya
kasri ya rais Kaskazini mwa jiji la Cairo kuonesha kuunga mkono uamuzi wa rais
huyo kujiongezea madaraka na kujiweka juu ya sheria za nchi
hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa
rais Morsi anatafakari kuhusu kuhutubia umma wa taifa la Misri baadye hii leo
kwa lengo la kutetea uamuzi wake.
Siku ya Alhamisi, rais alidhoofisha uwezo wa mahakama ambayo imekuwa ikifikiria kuweka usawa katika jopo linalotawaliwa na chama hicho cha kiislam kwa kutengeneza katiba mpya, kwa kuwaondolea majaji haki na mamlaka ya kuhoji kuhusu maamuzi yake.


Post a Comment