Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na wanachama wa CCM na CUF
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma kuanza ziara ya siku
mbili ya kichama Mkoani humo.
Makamu
wa kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad
akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mwenyekiti
wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba akiwahutubia
wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani
Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
--
Tanzania inahitaji
mabadiliko kwa kuwekeza katika kilimo cha kisasa sambamba na kutoa elimu na
huduma bora kwa wakulima ili waweze kuendeleza kilimo chenye
tija.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba
alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika
Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Amesema
Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutba inayokubali kuotesha mazao mbali
mbali, lakini bado hakujakuwepo na mikakati imara ya kuendeleza kilimo, jambo
ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa maslahi ya wananchi.
Prof.
Lipumba amefahamisha kuwa Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa inayoweza kufanya
vizuri katika kilimo kutokana na kuwepo kwa maziwa na mito ya kudumu ambayo
inaweza kutumika kwa kilimo cha mboga mboga na umwagiliaji, na kusaidia kukuza
kipato cha wakulima.
Sambamba
na hilo Prof. Lipumba amewataka wakulima kutilia mkazo mazao ya nafaka yakiwemo
mahindi na maharage, kutoka na kuongezeka kwa bei ya
mazao hayo katika soko la dunia.
Mwenyekiti
huyo wa CUF Taifa pia amesisitiza haja ya kuwepo kwa mikakati ya makusudi ya
kuongeza ajira kwa vijana ili kuwanusuru kujiingiza katika vitendo
viovu.
“Ukosefu
wa ajira unatisha, na ikiwa vijana hawana ajira wanaweza kushawishika kufanya
jambo lolote ambalo linaweza kuliletea madhara Taifa”, alifafanua Prof.
Lipumba.
Akizungumzia
kuhusu mchakato wa katiba, Prof. Lipumba ametaka katiba mpya ijayo itamke wazi
kuwa maliasili za Tanzania na mali ya Watanzania na iweke itaratibu ambao
Watanzania wataweza kunufaika na rasilimali hizo.
Amesema
iwapo wananchi watanufaika moja kwa moja na rasilimali
zao za nchi wataweza kuzilinda na kuziendeleza, lakini vyenginevyo rasilimali
hizo zinaweza kuleta maafa badala ya neema kama zilivyo baadhi ya nchi za Afrika
zikiwemo Nigeria na Equatorial Guinea.
Kwa
mujibu wa Prof. Lipumba Tanzania ina utajiri wa rasilimali mbali mbali zikiwemo
madini, mafuta na gesi asilia ambapo katika siku za hivi karibuni Kampuni moja
ya Norway iligundua gesi yenye futi za ujazo trilioni 5 katika kisima kimoja
pekee, ambapo jumla inakisiwa kuwepo na gesi trilioni 30 futi za
ujazo.
Amesema
rasilimaji zipo nyingi lakini zinahitaji kuwepo na uongozi wenye dira
utakaozingatia mgawanyo wa rasilimali
hizo kwa wananchi na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amesema CUF
kitasimamia sera yake ya haki na usawa, ili kuhakikisha kuwa kila Mtanzania
anapata haki zake za msingi zikiwemo za kisiasa, kiuchumi na huduma za
jamii.
Amesema
tatizo kubwa la Tanzania ni mipango duni ya kiuchumi, na kuwashauri wananchi
kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kurekebisha kasoro zilizopo na kuimarisha
uchumi wa nchi.
Kabla
ya mkutano huo, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,
aliupongeza uongozi wa Mkoa huo kutokana na ushirikiano mzuri wanaoutoa kwa
vyama vya siasa, na kwamba kufanya hivyo ni kuonesha ukomavu wa
kisiasa.
Katika
uwanja wa ndege wa Kigoma Maalim Seif alipokelewa na viongozi wa mkoa huo pamoja
na wafuasi wa CUF na Chama Cha Mapinduzi.
Mkutano
huo ni sehemu ya Operesheni mchakamchaka hadi 2015 iliyozinduliwa na chama hicho
kwa ajili ya kutembelea mikoa mbali mbali ya Tanzania kutoa uelewa kwa wananchi
ili hatimaye waweze kujiunga na chama
hicho.
Na
Hassan
Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza
wa Rais Zanzibar
Post a Comment