Mwezeshaji
katika mafunzo ya Ujasiriamali katika Wiki ya Ujasiriamali Duniani Austin Makani
(kushoto) akitambulisha meza kuu wakati wa Hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu
na kufunga Mafunzo hayo. Mgeni rasmi Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam Dkt. Ulingeta Mbamba (katikati), Mratibu Mipango wa Kitengo
cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDEC) Bw. Elia Yobu (kulia),
Makamu Mwenyekiti wa ZAYEE Bw. Omar Said Shabaan (wa pili kulia), Mkurugenzi
Mkuu wa Professional Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje (kushoto)
na Katibu Mkuu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la
ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) Fatma Mabrouk
Khamis (wa pili kushoto).
Pichani Juu na
Chini ni Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Dkt. Ulingeta Mbamba akitoa hotuba wakati wa kufunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa
Vijana yaliyoandaliwa na Asasi ya ZAYEE (Zanzibar Association for Youth
Education and Empowerment) na kutolewa na Kitengo cha Ujasiriamali cha Chuo
Kikuu cha DSM (UDEC).
Dkt. Mbamba
amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwa vijana kwa kuwa yatawawezesha kufanya
kazi zao kwa ufanisi, umahiri, tija zaidi na yatawasaidia sana katika kufanya
shughuli zao za kila siku ziwe za kujiajiri wenyewe au
kuajiriwa.
Katika mafunzo
hayo jumla ya vijana 103 (68 kutoka Dar es Salaam na 35 kutoka Zanzibar)
wamejifunza mambo mengi pamoja na Ujasiriamali, Fursa za Biashara zilizopo na
Changamoto zake, Jinsi ya kupata Wazo la Biashara pamoja na Mpango wa
Biashara.
Katibu Mkuu wa
ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akiwapa nasaha wakufunzi wa mafunzo ya
Ujasiriamali na kuwataka elimu waliyoipata hapo ikazae matunda katika kazi na
biashara wanazozifanya ili kuongeza tija itakayosaidia kukuza uchumi binafsi wa
Taifa.
Pia ameahidi
kuwafikia vijana wa Mikoani kuwapa mafunzo ya Ujasiriamali yatakayowezesha
kuimarisha biashara zao.
Mwenyekiti wa
Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education
and Empowerment) Bw. Masoud Salim Mohamed akizungumza na wahitimu hao ambapo
ametoa fursa kadhaa na kuwataka kujijengea utamaduni wa
kujiendeleza.
Mkurugenzi Mkuu
wa Professional Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje akizungumzia
umuhimu wa wajasiriamali kutumia michanganuo ya biashara katika kukuza biashara
zao.
Katibu Mkuu wa
ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akipokea cheti kufuzu mafunzo ya ujasiriamali
wakati wa wiki ya Ujasiriamali Duniani kutoka kwa Dkt. Mbamba ambayo kwa
Tanzania ndio mara ya kwanza kufanyika.
Pichani Juu na
Chini baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana jijini Dar es
Salaam.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kibo Palace
Hotel Charity Githinji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wahitimu wa
mafunzo ya Ujasiriamali jinsi ya kupata wazo la
biashara.
Wahitimu wa
Global Entreprenuership Week Tanzania katika picha kumbukumbu pamoja na mgeni
rasmi pamoja na wawezeshaji.
Bi. Fatma
Mabrouk Khamis (wa pili kushoto) na Mwakilishi kutoka ILO pamoja na baadhi ya
wahitimu.
Post a Comment