Ofisa wa utendaji na Mafunzo wa Jeshi la Wanamaji wa
Tanzanai Brigedia Jenerali Abdallah Athuman Mwemnjudi (kushoto) akitoa maelezo
jana (leo) jijini Dar es salaam kuhusu kuanza kwa zoezi liitwalo Cutlass Express
2 linaloshirikisha wanamaji kutoka Marekani, Msumbiji, Netherland na Tanzania
likiwa na lengo la kubadilishana uzoefu na mawazo juu ya kupambana na uharamia
katika mwambao wa Bahari ya Hindi. Kulia ni Kiongozi wa Kundi namba 1 la
wanamaji wa NATO Commodore Ben Bekkering.
*********************
Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dar es salaam
*********************
Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dar es salaam
Wanamaji kutoka nchi nne wameanza mazoezi nchini
Tanzania kwa ajili ya kubadilishana mbinu za kukabiliana na maharamia katika
mwambao wa Bahari ya Hindi. Madhumuni ya mafunzo hayo yanaendeshwa jijini Dar es
salaam ni kubadilisha uzoefu , elimu na mbinu za kukabiliana na vitendo vya
kiharamia ambavyo vimekuwa vikifanyika katika mwambao wa Bahari ya Hindi vya
utekaji wa Meli mbalimbali zikiwemo za mizigo . Kauli hiyo ilitolewa jana (leo)
jijini Dar es salaam na Brigedia Jenerali Abdallah Athuman Mwemnjudi wakati
akitoa ufafanunuzi kwa waandishi wa habari juu ya zoezi hilo la pamoja
linalozishirikiasha nchi mbalimbali lijulikanalo kama Cutlass Express 2. Alisema
kuwa zoezi hilo linalowashirikisha Wanamaji wa Jeshi la Marekani, Msumbiji,
Netherland na mwenyeji Tanzania litasaidia kuimarisha mapambano dhidi ya
Maharamia kwa kubadilisha uzoefu na kupeana taarifa ambazo zitawezesha Maharamia
kukamatwa kirahisi. Brigedia Jenerali Mwemnjudi alisema kuwa mafunzo
watakayopata wanamaji wa pande zote yatasaidia katika kuwajengea uwezo wa
kukabiliana na Mahamari katika hali yoyote na kuwana mbinu za Kimataifa za
kukabiliana na Uharamia. Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa suala ya
uharimia katika Mwambao wa Bahari ya Hindi kutoa Pembe ya Afrika hadi Msumbiji
ni salama kwa vyombo vyote vya majini na pia haitumiki kama njia ya biashara
haramu kama vile uvuvi haramu, usafirishaji wa binadamu, na usafirishaji wa dawa
za kulevya. Kuhusu hali ya Uharamia katika ukanda wa Afrika Mashariki Brigedia
Jenerali Mwemnjudi alisema kuwa hivi sasa matukio yameanza kupungua
ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo alitoa mfano kutoka mwaka 2010 hadi
mwanzani mwa mwaka huu kulikuwa na matukio zaidi ya 30 ya uharamia ambapo
maharamia 19 walikamatwa. Alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2012 ni tukio moja
lilitokea ambapo ni maharamia 12 walikamatwa. Brigedia Jenerali Mwemnjudi
alisema kuwa mara nyingi maharamia upenda kutenda uhalifu huo hasa kipindi cha
miezi ya kuanzia miezi Oktoba hadi Desemba wakati eneo la Bahari ni shwari.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo jijini Dar es
salaam.



Post a Comment