Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akihutubia
waumini wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT)
usharika
wa
Babati wakati wa
Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa hilo
Usharika wa
Babati,Mkoani Manyara leo.
Mbunge wa Jimbo la
Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni
(wa tatu
kulia)
akizungumza wakati
wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli
Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani
Manyara leo.Wengine
pichani toka Kushoto ni Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
(ambaye alikuwa mgeni
rasmi kwenye Harambee hiyo),
Mbunge wa Babati Mjini,
Kisyeri Chambiri na Kulia ni
Diwani wa kata
ya
Endamilay (CCM) Gesso
Bajuta.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akimpongeza
Mbunge wa Viti maalum Mkoani
Manyara (Chadema),Mh.
Pauline Gekul mara baada ya
kuchangia
kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli
Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,
Mkoani Manyara leo.Kulia
ni Mbunge wa Jimbo la
Babati Vijijini,Mhe.
Jitu Vrajlal Soni.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akiendelea kupokea
michango mbali mbali kwenye Harambee ya
Ujenzi wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika
wa Babati,Mkoani
Manyara leo.
Baadhi ya Waumini wa
Kanisa hilo wakiwa kwenye Harambee hiyo ya Ujenzi wa
Kanisa la Kiinjili la
Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,
Mkoani Manyara
leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh Edward Lowassa amesema wakati umefika sasa hapa
nchini elimu ya sekondari iwe ni elimu inayotolewa bure na kumwondolea mwananchi
mzigo .
Lowassa amesema hayo leo
mjini Babati wakati wa harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli
Tanzania (KKKT) usharika wa Babati.
Alisema kwa sasa kila
kata hapa nchini ina shule ya sekondari na huo ulikuwa mpango wake akiwa Waziri
Mkuu na alisimamia kikamilifu suala hilo na kufanikiwa kwa asilimia mia
moja.Shule hizo za kata ni maarufu kama shule za Lowassa.
Hata hivyo kiwango
kinachotolewa na shule hizo ni cha chini sana.
Waziri Mkuu huyo mstaafu
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli alisema sasa wakati umefika kwa kila
mtanzania kulizungumzia suala hilo bila ya woga hususani wadau wa elimu na
kuongeza kuwa.
''Ni lazima tukubali na
tujadili suala hilo kwa manufaa ya nchi kwa kila mtanzania kukubali ushauri huo
wa elimu ya sekondari kuwa ya bure''alisisitiza na kuongeza kuwa kuwa ni vyema
baada ya kulijadili suala hilo la elimu ya bure ya sekondari tena elimu iliyo
bora liwemo kwenye ajenda za Chama cha Mapinduzi (CCM) za uchaguzi mkuu wa
2015.
Lowassa alisema kuwa
hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alitoa wito kwa shule za sekondari kujenga
maabara kwa wingi,hivyo kwa hiyo amesema ni suala linalopaswa kuungwa mkono na
kila mtanzania na pia elimu ya bure katika sekondari nayo inapswa kuungwa
mkono.
‘’Nasema sasa wakati
umefika elimu ya sekondari kuwa kama elimu ya msingi kwa watoto kusoma bure
kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne ‘’alisema.

Post a Comment