Mrs Brdiget Katstriku ambaye ni Makamu wa Rais wa
AAPAM Afrika Magharibi akichangia mada katika Mkutano wa siku tano unoendelea
huko Zanzibar Beach Resort wa kujadili Ustawishaji huduma za jamii na utawala
bora (AAPAM) ,ikiwa leo nisiku ya pili ya Mkutano huo.
Proff.P.S Reddy,kutoka Chuo kikuu cha Kwazulu-Natal
akiwasilisha mada ya Usimamizi na tathmini ya utendaji kazi katika Manispaa ya
Afrika Kusini katika Mkutano wa siku tano unoendelea huko Zanzibar Beach Resort
wa kujadili Ustawishaji huduma za jamii na utawala bora kwa Nchi za
Afrika(AAPAM)
-Proff.P.S Reddy,kutoka
Chuo kikuu cha Kwazulu-Natal akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa wajumbe hawapo
pichani katika Mkutano wa siku tano unoendelea huko Zanzibar Beach Resort wa
kujadili Ustawishaji huduma za jamii na utawala bora kwa Nchi za
Afrika(AAPAM)
Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Na: Ramadhani Ali/Habari
Maelezo Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya
Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Joseph Meza ameeleza
kuwa Zanzibar itajifunza kwa kiasi kikubwa kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa
34 wa Kimataifa wa Jumuiya ya Nchi za Afrika wa Usimamizi wa Huduma za Umma na
Utawala bora (AAPAM) unaoendelea katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort
Mbweni.
Amesema Mkutano huo
unaowakutanisha wataalamu zaidi ya 500 wanaosimamia masuala ya Utumishi wa Umma
na Utawla Bora kutoka mataifa ya Áfrika, utawasadia sana viongozi wanaosimamia
sekta hiyo hapa Zanzíbar.
Meza amesema viongozi
wanaoshiriki mkutano huo wa situ tano, unaofanyika kwa mara ya kwanza
hapa Zanzíbar, wameonyesha wazi kuwa nchi zao zimepiga hatua kubwa katika
kusimamia huduma za utumishi wa umma na utawala bora, na imekuwa ni fursa nzuri
kwa washiriki wa Zanzíbar kujifunza kutoka kwao na kuleta mabadiliko ndani ya
taasisi za hapa nchini.
Pia amesema Mkutano huo
utaisaidia Zanzíbar kutangaza vivutio vyake vya utalii kwa vile wajumbe hao
watapata fursa ya kutembelea sehemu za mijini na mashamba na amewataka wananchi
kuonyesha ukarimu wao kwa wageni hao watakapo watembelea ili kupata picha halisi
ya nchi.
Akiwasilisha mada ya
utendaji bora katika kuimarisha huduma za jamii zinazotolewa katika nchi za
África, Makamu wa Rais wa AAPAM Afrika ya Kati Dk. Finlay Sama Doh
amesema suala la kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara wafanyakazi, kuwapa motisha
na kuimarisha vitendea kazi ni mambo yanayosaidia kwa kiasi kikubwa ufanisi
katika sekta za utumishi wa umma katika nchi.
Ameongeza kuwa suala la
kuwajengea utamaduni wafanyakazi kuheshimu sheria za kazi na kuwapa fursa ya
kujieleza wanapofikwa na matatizo ya kazi na kuyatafutia ufumbuzi ni miongoni
mwa vichocheo vya kuimarisha utawala bora na utendaji mzuri wa
kazi.
Ametoa wito kwa viongozi
wa Áfrika wanaosimamia masuala ya utumishi wa umma na utawala bora wanaoshiriki
mkutano huo kuweka mpango endelevu wa kufanya tathmini ya utendaji na
kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta hiyo katika nchi
zao.
Mkutano huo unatarajiwa
kumalizika Ijumaa ijayo na kabla ya kufungwa rasmi, viongozi wakuu wa AAPAM
watatangaza nchi mwenyeji wa mkutano ujao wa 35 wa Jumuiya
hiyo.

.jpg)
.jpg)
.jpg)

Post a Comment