Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWILI WA SHARO MILLIONEA UNAVYOONEKANA BAADA YA KUPATA AJALI YA GARI


Hivi ndivyo mwili wa sharo millionea ulivyokuwa baada ya kupata ajali
 ********

marehemu sharo Milionea amefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.
 
Hili ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.

 
Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

 
Akisimulia zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.





 
“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduka yeye alirushwa nje kupitia kioo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.








"Leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza Tanga mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei.

Taarifa hii imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga Constantine Massawe,
 

Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.

Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya utembeaji na uongeaji alipata Kunusurika katika ajali nyinge mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar es Salaam.
 
 

..... Kwa habari na picha zaidi, endelea kuperuzi NDGSHILATU BLOG nitakuletea .............
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top